UA-45153891-1

Friday, March 21, 2014

BONGO QUEEN LEO KATIKA SEMADAT


Leo tuko na mwanadada Hamisa  Hassan Mobeto ambaye anafanya jambo flani  kila mwaka juu ya fani yake ya mitindo tangu alipoanza mwaka 2010. Anatajwa na mtandao wa jarida la VIBE kama mtu wa kuangalia sana mwaka huu katika fani ya mitindo. Binti huyu mwenye umri wa miaka 21 ambaye  anatokea Mwanza , alianzia safari yake katika shindano ya XXL Back To School  ambapo aliibuka mshindi mwaka 2010. 
Baadae mwaka 2011 akashiriki shindano la Miss Dar Indian Ocean na kushika nafasi ya pili, pia mwaka huohuo aliibuka mshindi wa pili wa Miss Kinondoni na kuingia nusu fainali ya Miss Tanzania. Mwaka 2012 akashiriki Miss University Afrika na kuingia 10 bora. Kama ukitazama video ya muziki ya wimbo wa My Baby wa Quick Racka utamuona alivyotumia kipaji chake kama Video Vixen. Mwanzoni mwa mwaka huu 2014 ametokea kwenye ‘Cover’ ya mbele  ya jarida la Pulse la nchini Kenya.

1 comment:

  1. The 10 best casinos of 2021 - Yak Casino
    There is no doubt that Jackpot City Casino is the best place to play. It 1XBET has the latest dafabet slots 12bet and table games, as well as a live casino

    ReplyDelete