UA-45153891-1

Tuesday, March 4, 2014

KARABANI, DJ NA MWANAMUZIKI ALIYEBADILIKA KUWA DIRECTOR WA FILAMU NCHINI TANZANIA

Karabani

“Mwanzoni ilikzuwa kama hobi. Tangu nikiwa mdogonilipenda sana filamu lakini sikufikilia kufanya kazi hii mpaka nilipojihisi kuuchoka  muziki”.  Anasema ‘Director’ huyo ambaye pia ni mtayarishaji wa filamu. Karabani ambaye mwanzoni alikuwa DJ, na baadae mtayarishaji wa muziki, aliona haitoshi na  kuanza utayarishaji wa video za muziki pia. 

Karabani ambaye amesomea Uchumi na Biashara, aliendelea kufanya  hayo kuhusiana na muziki lakini hakufanikiwa zaidi ya kukuza  ujuzi  na uzoefu wa mambo hayo. Baada ya hapo alianzisha ‘show’ kwa njia ya ‘internet ‘ kupitia mtandao wa Youtube ambapo yeye mwenyewe alikuwa  anafanya kazi kama  Host, Producer  na Editor. Kila kitu alifanya yeye ambapo aliweka kamera na mbele yake na kuanza kuongea. Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wake kwenye tasnia ya  filamu.


Ni muongozaji wa filamu na anashiriki katika mradi wa Swahiliwood, ambapo ameongoza filamu ya Sunshine iliyozinduliwa Februari  20, 2014.


No comments:

Post a Comment