UA-45153891-1

Wednesday, March 5, 2014

JACKSON KABIRIGI ANAVYOIZUNGUMZIA ‘SWAHILIWOOD’ NA MWELEKEO WA SANAA YA FILAMU NCHINI TANZANIA

Jackson Kabirigi

Jackson Laulent Kabirigi ni muongozaji  wa filamu ‘Director’ aliyeongoza filamu ya ‘Mdundiko’ ambayo imemtangaza sana hapa nchini, Marekani na pande mbalimbali za dunia. Filamu hiyo iliyompa heshima kubwa , iliandaliwa chini ya mradi wa Swahiliwood .


“Kila wakati natamani kuwapa mkono watu walioleta Swahiliwood,nawashukuru mara elfu moja.  Kwa kusema ukweli, nilipoanza kushiriki kwenye mradi wa Swahiliwood watanzania wengi waliniuliza “Ni kitu gani kizuri juu ya mradi huo?,  wanataka kutuletea nini? na wanafikili wanaweza kutusaidiaje?” lakini mafanikio ni makubwa. Binafsi nimejifunza mengi”, anasema Kabirigi.

“Washiriki wengine hata kama pengine bado hawajashinda tuzo lakini sote tumejifunza. Naamini kiwanda cha filamu nchini Tanzania kitabadilika na chanzo cha mabadiliko hayo ni Swahiliwood. Soko la filamu nchini Tanzania halikui kwa kasi vile inavyotakiwa lakini mradi kama Swahiliwood unatufanya kuelewa nia hatua gani tuchukue na tufanye nini  kufanikiwa. Tukichukua hatua sahihi tunaweza kulifikia hata soko la Marekani.  Nilishangaa sikutegemea kama ‘Mdundiko’ ingefahamika Marekani . Hii inanionyesha kwamba filamu zetu zinaweza  kwenda mbali. Moja ya vyanzo  vya haya yote ni kitu kama Swahiliwood”, alinukuliwa Jackson  Kabirigi kupitia kipeperushi cha utambulisho wa filamu ya ‘Mdundiko’.

Kabla Kabirigi hajaanza shughuri za filamu alikuwa kwenye sanaa ya muziki kama muimbaji na baadae akaanza kushughurika na video za muziki, ndipo  alipovutiwa na filamu kwa ujumla. Pia alipata hamasa kubwa kutoka kwa watu aliofanya nao kazi mwanzoni ambao walimwambia anaweza  kufanya vizuri baada ya kufurahishwa sana na mawazo yake wakati wa shughuri za maandalizi ya filamu.

Jackson Kabirigi alizaliwa mkoani Kagera na ameanza kufanya kazi za sanaa Dar es Salaam mwaka 2003. Wazazi wake ni wakulima na yeye ni mtoto wa tatu katika familia ya watoto saba. Alipata tuzo katika tamasha la filamu za Afrika la Silicon Valley mwaka 2013 nchini Marekani  kutokana na filamu ya ‘Mdundiko’.
                                                                                                                                                                     

No comments:

Post a Comment