UA-45153891-1

Tuesday, March 11, 2014

HAPPY BIRTHDAY DIDIER DROGBA

Mcheza soka maarufu wa barani Afrika anayetokea nchini Ivory Coast, Didier Drogba ametimiza umri wa miaka 36 leo Machi 11, 2014. Mchezaji huyo ‘striker’ ambaye ndiye aliyekuwa mchezaji wa kwanza aliyezaliwa Afrika kufunga magoli 100 kwenye mashindano ya UEFA na ambaye alikuwa miongoni mwa wachezaji waliofunga magoli mengi katika historia ya timu ya Chelsea, alianza mikiki ya soka akiwa na umri wa miaka 18 aliposaini mkataba na Levallois.

Alikuwa mwanasoka bora wa Afrika mwaka 2006, 2009 na 2012 huku akipigiwa kura na mashabiki wengi wa Chelsea kama mchezaji bora wa Klabu hiyo.

Drogba ana watoto watatu na mke wake Diakite Lalla ambaye walioana Juni 11, 2011. Ana wadogo zake wawili wa kiume Joel na Freddy Drogba ambao pia wanacheza  soka. Miongoni mwa wachezaji aliocheza nao soka timu moja kwa muda mrefu ni pamoja na Frank Lampard ambaye walikuwa wote Chelsea kuanzia 2004 to 2012.

No comments:

Post a Comment