UA-45153891-1

Tuesday, March 4, 2014

ELOHOR AISIEN ASEMA ‘GOODBYE’ KWA MASHINDANO YA ‘MISS NIGERIA’

Elohor Aisien
 
Aliyekuwa muandaaji wa shindano ya Miss Nigeria Elohor Aisien chini ya kampuni ya The Elite Model Look, ameachia ngazi na kuachana na uandaaji wa shindano hilo ili kuwekeza nguvu zaidi katika kuandaa matukio ya kifahari zaidi chini ya kampuni yake inayoitwa ‘Prive’. Bi. Elohor Aisien alikabidhiwa haki za ubunifu na utawala na timu ya ‘Miss Nigeria’ July 2012 na kufanikiwa kuandaa shinano la Miss Nigeria 2013 lililowezesha kumpata mrembo Ms Ezinne Akudo.

Kampuni yake mpya ya Prive iliyozinduliwa mwaka 2013 inahudumia chakula katika matukio makubwa sana nchini humo na ratiba yake ni ngumu sana ambayo inahitaji uwepo wake kama kiongozi. Pamoja na hivyo ameshapanga kuonana na wataalam wa masuala ya urembo na mitindo kutoka Ulaya ili wasimamie kampuni yake ya Elite model look kuanzia mwaka huu wa 2014.

No comments:

Post a Comment