UA-45153891-1

Friday, March 21, 2014

RONALDINHO ‘GAUCHO’ ATIMIZA MIAKA 34 (HAPPY BIRTHDAY GAUCHO)


Mwanasoka maarufu wa nchini Brazil ambaye mwanzoni mwa mwaka huu alisema atakapoachana na mchezo wa Soka ataingia kwenye sanaa ya muziki, Ronaldinho ‘Gaucho’ anasherehekea siku yake ya kuzaliwa leo Machi 21, 2014 ambapo anatimiza miaka 34.

Mwanasoka huyo amechezea timu yake ya Taifa ya Brazil na timu mbalimbali ikiwa pamoja na  Barcelona. Kabla hata hajajulikana katika ulimwengu wa soka, alipewa jina la utani la ‘El Gaucho’ akiwa na umri wa miaka 8 kwa sababu alionekana mdogo kwa kulinganishwa na watu aliokuwa akionekana nao muda mwingi.

Ronaldinho alipata mtoto  akiwa na umri wa miaka 25 baada ya mcheza muziki ‘Dancer’ wa nchini Brazil aitwaye Janaina Mendes kujifungua mtoto wake anayeitwa Joao.

No comments:

Post a Comment