Rostam Azizi
Kabla ya hapo, mara ya mwisho tulimfahamu kama mmoja kati ya matajiri wakubwa barani Afrika na tajiri wa kwanza nchini Tanzania lakini hakuwa bilionea. Sasa anabaki katika orodha hiyo lakini pia akiwa tayari ni bilionea.
Rostam Azizi amekuwa mtanzania wa kwanza kutangazwa na Jarida la Forbes kama bilionea mpya kutoka Afrika. Rostam ambaye ametangazwa kwenye orodha iliyotoka mwaka huu 2014 ndani ya mwezi Machi, anamiliki asilimia 35 ya hisa za kampuni ya simu ya ‘Vodacom Tanzania’, mtandao wa simu wenye wateja zaidi ya milioni 10, pia anamiliki kampuni ya madini ‘Caspian Mining’ inayotoa huduma kwa makampuni makubwa kama BHP Billiton and Barrick Gold. Kampuni yake ya ‘Caspian Mining’ pia inamiliki vitaru vya uchimbaji wa madini ya Dhahabu, Shaba na Chuma nchini Tanzania.

Mbali na hapo, amewekeza katika bandari ya Dar es Salaam akiwa ni sehemu ya kampuni ya Hong Kong ‘Hutchison Whampoa’. Yuko pia katika biashara ya habari upande wa magazeti na biashara za ardhi na majengo ‘Real Estate’ nchini Tanzania, Dubai, Oman na Lebanon. Pia alikuwa Mbunge wa Tanzania. Hii yote ni kwa mujibu wa mtandao maarufu wa Forbes ambao pia wanasema Rostam Aziz hutoa mamilioni ya pesa kila mwaka kusaidia makundi maalum upande wa elimu, afya na utamaduni.
No comments:
Post a Comment