Si kweli kwamba kuna mtu ambaye hapendi kupata mafanikio, ila ukiona alama hizi kumi kwako basi ujue unatakiwa kuwa makini.
1. Kungoja usifiwe au unachokifanya kikubaliwe na wengine
Unapofikia hatua ya kufanya maamuzi muhimu juu ya kuchagua unachataka kufanya ukayapa thamani kubwa mawazo ya wengine zaidi ya yako ni dalili ya kutohitaji mafanikio. Watu wengi wenye mafanikio makubwa hawafanyi kwa mawazo ya kila mtu au hata mtu yeyote bali kile wanachohisi kwamba ndicho kitakachofanya watimize ndoto zao.
2. Unajiburudisha zaidi kuliko unavyojielimisha
Unafanya kazi nzuri, lakini hujawai kufungua kitabu chochote kusoma, kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu ujuzi na taaluma yako kwa njia ya intaneti, kusikiliza ‘podcasts’ au kuuzulia semina yoyote zaidi chuo ulichosomea au mafunzo uliyopata wakati unaanza kazi.
3. Unawalaumu wengine kwa matokeo ya maamuzi yako mwenyewe
Unaishia kumlaumu bosi wako, wafanyakazi wenzako, wazazi wako, elimu au taaluma yako, utoto au ujana wako na uchumi wako badala ya kuchukua hatua. Unashindwa kukubali kwamba unajiongoza katika maisha na unatakiwa kuifuata njia uliyoichagua.
4. Unaogopa kukosea
Unaogopa kufanya makosa hivyo kwa kila ufanyalo unajitaidi kuweka kinga ya kukosea, unasahau kwamba katika Ulimwengu halisi kukosea si kuzuri wala kubaya bali ni matokeo. Badala ya kutumia matokeo hayo kujifunza unajaribu kuyazuia kabisa matokeo yake unashindwa hata kufanya maamuzi kwa kuwa unaogopa kufanya yale yasiyokuwa sahihi.
5. Unatumia muda mwingi na watu wasiokupeleka popote
Mwanafalsafa mmoja wa kibishara kwa jina la Jim Rohn alisema “Unakuwa wastani wa watu watatu unaotumia muda mwingi ukiwa nao”, Kwa bahati mbaya labda unatumia muda wako na watu ambao hawakupi moyo juu malengo yako, watu waliokuzunguka, wakati mwingine unazungumza nao juu ya ndoto zako lakini wanakukatisha tamaa.
6. Haujari matumizi mazuri ya pesa
Unatumia pesa katika hali ya kukufanya uonekane umefanikiwa wakati salio lako linazungumza stori nyingine, hauko tayari kuwekeza kwa njia yoyote wala mpango wa lolote la kufanya utakapostaafu.
7. Una ndoto kubwa lakini hakuna malengo yoyote uliyojiwekea
Mambo unayowazia bado ni ya kufikilika tu, badala ya kufanya kazi ili yabadilike kuwa ukweli, unatulia tu, unasema unahitaji maisha flani au kitu flani lakini hufanyi chochote kutafuta. Watu wenye mafanikio hujitoa na kusimamia malengo ambayo tayari wameyapanga. Hii ni pamoja na maamuzi na shughuri za kila siku wazifanyazo kuelekea huko.
8. Unaishi katika mahusiano yasiyokufaa
Uko katika mahusiano ya kimapenzi ambayo yanakuletea zaidi matatizo zaidi ya furaha unavumilia tabia ambazo unajua hazikubaliki na kwa kuwa unazivumilia zinaendelea. Pengine unakutana na yaleyale uliyoyakutana nayo katika uhusiano uliopita na hayakutatuliwa, kwa vyovyote vile ufanyavyo lazina uelewe kwamba chaguo la mwenza wako lina matokeo makubwa katika maisha yako.
9. Kuishi maisha ya visasi na chuki
Kutokuwa mtu wa kusamehe, kusahau yaliyopita na kusonga mbele, kusengenya au kunyooshea vidole wengine. Kujenga hisia juu ya watu wanazungumza nini juu yako badala ya kuziona kama changamoto kuongeza mwendo.
.
10 . Kufikiri waliofanikiwa wamefanikiwa kwa bahati
Kwamba labda wazazi wao waliwasaidia kifedha, walikwenda shule ambayo ni nzuri zaidi, walikulia katika mazingira ya kuwafanya wawe hivyo, waliingia mapema kwenye biashara au kazi husika, au walimfahamu mtu flani. Si kweli, ila tu ni kwamba wanajiandaa kwa ajili ya jambo flani na nafasi inapotokea wanaitumia vizuri.
No comments:
Post a Comment