Abdul simba ni mwandishi wa script za fimamu ambaye yuko kwenye mradi wa Swahiliwood unaofanya shughuri za utayarishaji wa filamu kwa hisani ya watu wa Marekani kupitia USAID kwa kushirikiana na kituo cha mawasiliano cha Chuo kikuu cha John Hopkins pamoja na Proin Promotions ambao ni wasambazaji wa DVD.Haya ni mambo kumi kuhusu mwandishi huyo:
1. Ana miaka kumi sasa tangu aanze kufanya kazi hiyo.
1. Ana miaka kumi sasa tangu aanze kufanya kazi hiyo.
2. Alijifunza mwenyewe kwa kuwa alipenda sana kuandika stori na alitumia muda wake mwingi kuatazama filamu za aina mbalimbali.
3. Ndoto ilianzia alipotamani kukibadilisha kuwa filamu kitabu cha ‘Things Fall Apart ‘ kilichoandikwa na mnigeria Chinua Achebe.
4. Amesomea mambo ya Historia, Siasa na Falsafa nchini Uingereza.
5. Dira yake kuu ni kuwaenzi waandishi wa Tanzania na Afrika nzima kwa kufanya kazi zao zikumbukwe kupitia filamu.
6. Alipata hamasa kubwa kutoka kwa dada yake ambaye pia alikuwa kwenye sanaa ya muziki ,filamu na uandishi wa vitabu.
7. Hatua ya kwanza ilianzia mwaka 2004 pale alipopata nafashi kushiriki kwenye ‘Maisha Screen Lab’ jijini Kampala, chini ya Muongozaji wa filamu wa nchini India ‘Mira Nair’ ambaye alimwambia anaweza kuandika.
8. Anaiona gharama ya teknolojia kama changamoto kubwa kwenye utayarishaji na matumizi ya filamu.
9. Ameandika Script ya filamu ya Sunshine, moja ya filamu mpya kutoka Swahiliwood.
10. Mama yake ni mchanganyiko wa kichaga na kisomali na baba yake mchanganyiko wa Kigoma na Rufiji.
Shkamooo...nataka kuusajili mswada Wangu kabla ya kuuza-je! Ni lazima? Kama ni lazima /muhimu: nasajilia wapi? Tafadhali nijibu.
ReplyDeletegoodbeatus92@gmail.com