UA-45153891-1

Thursday, March 20, 2014

SIKU YA FURAHA YA KIMATAIFA (INTERNATIONAL DAY OF HAPPINESS, 20 MARCH 2014)


"Furaha inaweza kuwa na maana tofauti kwa watu tofauti lakini wote tunaweza kukubaliana kwamba inamaanisha kufanya kila linalowezekana kumaliza migogoro, umasikini na hali zingine mbaya ambazo binadamu wenzetu wengi wanaishi nazo".  Ni ujumbe kutoka kwa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa  Ban Ki-moon, katika siku hii ya furaha duniani Machi 20, 2014.

Hebu jaribu kutafakari ni nani hana furaha kutokana na sababu moja au nyingine na ungependa awe nayo.Bila shaka utakuwa mmoja wa wale wanaofurahi pindi wawaonapo wengine wakifurahi. Semadat inakutakia furaha na hali ya kuendelea kuikaribisha furaha kuanzia siku ya leo. 'Happy International Day of Happiness'.

No comments:

Post a Comment