Madee
Baada ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kutangaza majina ya wanamuziki na nyimbo zilizoingia kwenye tuzo za muziki za Kilimanjaro, ikiwa ni pamoja na kuwataja wasanii ambao nyimbo zao hazikupata nafasi hiyo kutokana na sababu za kimaadili, wasanii hao wamesikika kupitia vyombo vya habari wakitoa maoni yao juu ya suala hilo.
Wa kwanza alikuwa Madee ambaye alisema chombo husika kimefanya kazi yake japo haikuwa vema kuchukua hatua hiyo katika hatua za tuzo wakati nyimbo ziliruhusiwa kuchezwa Redioni na video zake kuonyeshwa katika Televisheni. Aliwaomba Basata kuchukua hatua mara moja pindi waonapo lolote ambalo liko kinyume na maadili maana kuna gharama kubwa zinatumika kuandaa kazi hizo na pia kufanya promosheni. Madee alisema alisikia maneno muda mrefu juu ya suala la wimbo wake 'Tema mate tuwachape' lakini hakupata barua rasmi kutoka Basata, nae akaendelea kuupa nguvu wimbo huo.
Snura
Pia amesikika Snura ambapo yeye amezungumzia tofauti kati ya wimbo na video ya wimbo.Amekubali kwamba inawezekana video ya wimbo wake wa 'Nimevurugwa' haikustaili kutokana na jinsi alivyocheza, lakini maudhui ya wimbo hayana ubaya wowote. "Kwa kuwa kuna kipengele cha video na vipengele vya wimbo, hakukuwa na sababu ya kuachana nao kabisa badala yake ungeweza kukosa kipengele cha video na kuingia vipengele vingine", amesema Snura.
Msemaji wa Basata alikubaliana na ushauri wa Madee kwamba ni kweli walichelewa lakini ni changamotoa za hapa na pale kuelekea urasimishaji wa muziki ambapo kila wimbo utakuwa ukiwafikia kabla hata ya kurushwa hewani na vyombo vya habari.
Nyimbo zilizokosa nafasi hiyo kwa sababu za kimaadili ni "Tema mate tuwachape" wa Madee, "Nimevurugwa" wa Snura na "Uzuri wako" wa Jux.

No comments:
Post a Comment