UA-45153891-1

Monday, March 3, 2014

LUPITA NYONG’O ASHINDA TUZO YA OSCAR KUPITIA FILAMU YA “12 YEARS SLAVE”



Muigizaji maarufu wa kike wa nchini Kenya ambaye anafanyia shughuri zake za filamu Hollywood nchini Marekani, ameshinda tuzo ya Oscar kwenye tuzo hizo za 86 za Academy kwa uhusika wake katika filamu ya 12 Years a Slave ambayo ilitengenezwa mwaka 2013 chini muongozaji Steve McQueen.

Ameshinda tuzo hiyo kipengele cha ‘Best supporting actress’ ambapo alikuwa anachuana na mastaa wengine wakubwa akiwemo Sally Hawkins wa filamu ya Blue Jasmine na muigizaji maarufu wa nchini Marekani Jennifer Lawrence.



Filamu ya 12 Years a Slave iliyompatia Lupita tuzo hiyo, ina dakika 133 ilifanyika nchini Marekani na sehemu  mbalimbali za nchi tofauti. Lupita Nyong’o ambaye alizaliwa nchini Mexico na kukulia katika nchi yake ya Kenya, inakuwa filamu yake ya kukumbukwa ambayo ni ya kwanza kucheza kama muhusika mkuu.




No comments:

Post a Comment